Anthems 1
Ee Mungu Nguvu Yetu
1Ee Mungu nguvu yetu,
Ilete baraka kwetu.
Haki iwe ngao na mlinzi,
Natukae na undugu,
Amani na uhuru,
Raha tupate na ustawi.
2Amkeni ndugu zetu,
Tufanye sote bidii,
Nasi tujitoe kwa nguvu,
Nchi yetu ya Kenya Tunayoipenda,
Tuwe tayari kuilinda.
3Natujenge taifa letu,
Ee ndio wajibu wetu,
Kenya istahili heshima,
Tuungane mikono Pamoja kazini,
Kila siku tuwe na shukrani.