Skip to content

Nyimbo za Kristo 106

Huna Kitu Kwa Yesu

Have You Any Room for Jesus?

Tune: Christ in Song 100

1Ukitafuta mali,
Huna wasaa kwa Yesu?
Kwa matendo ya haki
Huna wasaa kwa
Yesu‿Anasa za dunia,
Mambo yako ya raha
Haya‿unatafuta;
Huna wasaa kwa Yesu?

2Mambo yanakusonga:
Kwake huna nafasi?
Watekwa na dunia,
Kwake huna nafasi?
Humwona m-langoni,
Anapopiga hodi?
Daima hukusihi:
Kwake huna nafasi?

3Sa-a ni za thamani,
Kwake hamnayo kazi
Wala hamfanyi bidii,
Kwake hamnayo kazi?
Hamkufikia kwao Waliomo shimoni
Na waliopotea?
Kwake hamnayo kazi?

4Na wazaa majani tu?
Huna tunda kwa Yesu?
Mikono‿I mitupu,
Huna tunda kwa Yesu?
Huna chembe kwa ghala
Kazi yako kulipa;
Wala huna furaha
Unapomwona Yesu?