Skip to content

Nyimbo za Kristo 132

Bwana Ni Mchunga

The Lord's My Shepherd

Tune: Church Hymnal 405

1Bwana ni Mchunga,
Sitahitaji;
Majani mabichi malisho yangu.
Ananinywesha maji matulivu;
Atanirudisha nikipotea.

2Nipitapo bondeni mwa mauti
U mlinzi wangu sitaogopa;
Fimbo lako latosha kunilinda;
Ukinifariji sina hasara.

3Kati ya mateso meza waandaa,
Na kikombe changu kinafurika‿Umenipaka kichwani mafuta;
Nitaulizaje zaidi kwako?

4Wema na fadhili zinifuate
Siku zangu zote hata milele;
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana
Katika‿ufalme wa pendo lake.