Skip to content

Nyimbo za Kristo 54

Nataka Nimjue Yesu

Studio

1Nataka nimjue Yesu, na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake tu, wokovu wake kamili.

RefrainZaidi, zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue upendo wake, wokovu wake kamili.

2Nataka nione Yesu, na nizidi kusikia Anenapo kitabuni, kujidhihirisha kwangu.

3Nataka tena zaidi, daima kupambanua Mapenzi yake, nifanye yale yanayompendeza.

4Nataka nikae naye, kwa mazungumzo matamu.
Nizidi kuwaonyesha wengine wokovu wake.