Skip to content

Nyimbo za Kristo 108

Tumesikia Mbiu

Studio

1Tumesikia mbiu:
Yesu huokoa;
Utangazeni kote,
Yesu huokoa;
Tiini amri hiyo: nchini baharini.
Enezeni mbiu hii:
Yesu huokoa.

2Imba nawe askari:
Yesu huokoa;
Kwa nguvu ya kombozi,
Yesu huokoa;
Imbeni wenye shida, unapoumwa moyo,
Na kaburini imba:
Yesu huokoa.

3Mawimbini uenee.
Yesu huokoa;
Wenye dhambi jueni:
Yesu huokoa;
Visiwa na viimbie, vilindi itikeni,
Na nchi shangilie:
Yesu huokoa.

4Upepo utangaze:
Yesu huokoa;
Mataifa yashangaa:
Yesu huokoa;
Milimani, bondeni, sauti isikike Ya wimbo wa washindi:
Yesu huokoa.