Nyimbo za Kristo 140
Hivi Nilivyo Unitwae
Just as I Am
Tune: Church Hymnal 222
1Nitwae hivi nilivyo, umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita,
Bwana Yesu, sasa naja.
2Hivi nilivyo; langu kujiosha roho yangu;
Nisamehe dhambi zangu,
Bwana Yesu, sasa naja.
3Hivi nilivyo; sioni kamwe furaha moyoni,
Daima ni mashakani,
Bwana Yesu, sasa naja.
4Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu;
Wewe ndiwe u tajiri,
Bwana Yesu, sasa naja.
5Hivi nilivyo, mimi tu,
Siwezi kujiokoa;
Na wewe hutanikataa,
Bwana Yesu, sasa naja.
6Hivi nilivyo; mapenzi yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi,
Bwana Yesu, sasa naja.