Nyimbo za Kristo 141
Chini Ya Msalaba
1Chini ya msalaba Nataka simama;
Ndio mwamba safarini,
Wa kivuli chema;
Ni kweli kwa roho yangu Ni tuo kamili,
Tatua mzigo wangu Wakati wa hari.
2Hapa ni pema sana,
Ni ngome kamili;
Hapa yameonekana,
Mapenzi ya kweli;
Kama alivyoonyeshwa Yakobo zamani.
Msalaba umekuwa Ngazi ya mbinguni.
3Na Yesu Msalabani Walimkemea,
Alikufa niokoke Niliyepotea:
Naona ajabu sana Ya mambo mawili Jinsi alivyonipenda Nisiyestahili.
4Atakayeonana Na Yesu mbinguni,
Njia yake aanzapo Ni Msalabani;
Wokovu upo hapa tu,
Mwingine hapana.
Kisha kuna furaha kuu Pamoja na Bwana.