Skip to content

Nyimbo za Kristo 15

Nena Mungu

Speak to My Soul, Dear Jesus

Tune: Christ in Song 554

1Nena rohoni Yesu,
Nena kwa upole
Sema kwangu kwa pendo,
"Huachwi upweke." Fungua moyo wangu,
Nisikie mara;
Jaza roho na sifa,
Sifa zako Bwana.

RefrainKila siku unene,
Vile kwa upole,
Nong'oneza kwa pole wa pendo:
"Daima utashinda,
Uhuru ni wako."
Nisikie maneno; "Huachwi upweke."

2Nena kwa wana wako, waonyeshe njia,
Wajaze kwa furaha,
Fundisha kuomba;
Wajifunze kutoa Maisha kamili,
Wahimize ufalme,
Tumwone mwokozi.

3Nena kama zamani,
Ulipoitoa Sheria takatifu:
Niiweke pia;
Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu,
Mapenzi yoko tena,
Daima kusifu.