Skip to content

Nyimbo za Kristo 16

Ninakuhitaji

Tune: Church Hymnal 578

1Bwana ninakuhitaji!
Ni mpofu, maskini;
Unishike mkononi,
Kwako napata nguvu.

RefrainKila saa, kila saa Bwana ninakuhitaji;
Kila saa, kila saa‿Unilinde kila saa.

2Univike na mavazi
Ya usikivu wako;
Nguo zangu ni machafu,
Nazitamani zako.

3Wewe ukiniongoza Nitakwenda salama;
Nenda nami siku zote,
U nuru na uzima.

4Na ikiwa m-beleni
Sehemu yangu ngumu,
Au ikiwa furaha,
Unilinde kila saa.