Skip to content

Nyimbo za Kristo 164

Mishale Ya Nuru

Studio

1Unakaribia wakati wa Kuja kwa Yesu.
Atawachukua watu wake Nyumbani juu.

RefrainTunaiona mishale ya nuru Inayopenya giza;
Tunaiona mishale ya nuru Ya ufunuo.

2Injili inatangazwa pote kwa mataifa;
Bwana wa Arusi atakuja Na tarumbeta.

3Pamoja na malaika zake Bwana arudi,
Awapeleke waaminifu Wasife tena.

4Wapenzi waliotengwa kale Watakutana;
Machozi yao wenye huzuni Yatafutika.

Mishale Ya Nuru – Nyimbo za Kristo 164 lyrics | Advent Hymnals