Skip to content

Nyimbo za Kristo 176

Ati Tuonane Mtoni

Studio

1Ati tuonane mtoni?
Maji mazuri ya mbingu;
Yanatokea mwangani, penye kiti cha Mungu.

RefrainNaam, tuonane mtoni!
Watakatifu, kwenu ni mtoni!
Tutakutanika kule mtoni penye kiti cha Mungu.

2Tukitembea mtoni na Yesu Mchunga wetu,
Daima tu ibadani usoni pake kwetu.

3Tukisafiri mtoni tutue ulemeao Wema wa Mungu yakini; una taji na yao!

4Kwang'ara sana mtoni cha Mwokozi ni kioo,
Milele hatuachani tumsifu kwa nyimbo.

5Karibu sana mtoni, karibu tutawasili,
Mara huwa furahani na amani ya kweli.