Nyimbo za Kristo 175
Uso Kwa Uso
1Nitaonana na Yesu, uso kwa uso kweli;
Siku ile shangwe tele nikimwona Mwokozi.
RefrainTutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni;
Na kwa utukufu wake nitamwona milele.
2Sasa siwezi kujua jinsi alivyo hasa,
Bali atakapokuja, nitamwona halisi.
3Mbele yake yafukuzwa machozi na huzuni;
Kipotovu kitanyoshwa, fumbo litafumbuka.
4Uso kwa uso!
Hakika palepale furaha;
Nitafurahi kabisa nikimwona Mwokozi.