Nyimbo za Kristo 178
Ukingoni Mwa Yordani
On Jordan's Stormy Banks
Tune: Church Hymnal 553
1Ukingoni mwa Yordani ninaangalia
Bara nzuri ya
Kanaani, ninayotamani.
RefrainTutakaa pamoja na Yesu,
Katika pwani yenye raha;
Tutaimba wimbo wa Musa na Kondoo,
Milele hata milele.
2Bara ile ina nuru, nuru ya milele;
Kristo,
Jua, hutawala, hufukuza giza.
3Nitapafikia lini na kubarikiwa,
Penye ufalme wa Baba, na kumwona uso?
4Furaha yangu rohoni ni kuchukuliwa;
Siyaogopi mawimbi katika Yordani.