Nyimbo za Kristo 177
Kazi Yangu Ikisha
My Savior First of All
Tune: Christ in Song 849
1Kazi yangu ikisha, nami, nikiokoka,
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua Mwokozi; nivukapo ng'amboni
Atakuwa wa kwanza kunilaki.
RefrainNitamjua, nitamjua,
Nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua,
Kwa alama za misumari.
2Kuona uso wake kutanipa furaha,
Furaha isiyo ya kukomesha;
Nitamsifu Mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyonipa pahali mbinguni.
3Nao waliokufa katika Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko mbinguni,
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
4Milangoni mwa mji Bwana atanipisha,
Pasipo machozi wala huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele: lakini
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.