Nyimbo za Kristo 180
Pana Mahali Pazuri Mno
Sweet By and By
Tune: Church Hymnal 551
1Pana mahali pazuri mno,
Twapaona kwa mbali sasa;
Baba yetu‿angoja pale,
Amepanga makao yetu.
RefrainKitambo tu bado,
Tutakutana ng'ambo pale.
Kitambo tu bado,
Tutakutana ng'ambo pale.
2Tutaimba pale kwa moyo
Nyimbo tamu za wenye heri.
Na rohoni hatutaona
Tena haja ya kupumzika.
3Kwa baba yetu mkarimu
Tutatoa shukrani sana.
Kwa kipaji cha pendo lake
Na baraka anazotupa.