Nyimbo za Kristo 184
Panapo Pendo
1Vitu vyote ni sawa, panapo pendo:
Kila sauti tamu, panapo pendo;
Pana amani pale, na furaha nyumbani,
Siku zote salama panapo pendo.
RefrainPanapo upendo;
Siku zote salama panapo pendo.
2Furaha i nyumbani, panapo pendo:
Hapana machukizo, panapo pendo;
Chakula ni kitamu, mashamba yasitawi,
Maisha ni kamili, panapo pendo.
3Hata mbinguni juu pana furaha Wakiona upendo nyumbani mwetu.
Macho yapendezwa na viumbe vya Mungu,
Naye Mungu huona, panapo pendo.
4Ee Yesu niwe wako, wako kabisa,
Ndipo patakuwako Pendo nyumbani;
Nitakaa salama, sitafanya dhambi Nitabarikiwa tu panapo pendo.