Skip to content

Nyimbo za Kristo 185

Mungu, Mapenzi Makamilifu

Studio

1Mungu u mapenzi mtakatifu Yapitayo fahamu za watu Twanyenyekea sisi wapungufu,
Wape baraka wapenzi wetu.

2Ewe Mapenzi yasiyopimika Twawaombea kitini Mwako,
Wape mapenzi yasiyotindika,
Waliooana mbele yako.

3Ewe uhai, wewe u dhamana Ya imani na matumaini,
Wape kuvumilia hapa sana Wasiche maumivu mwishoni.

4Wape furaha hiyo iwezayo kutia nuru kwenye huzuni,
Wape amani hiyo itakwayo Katika matata duniani.

5Waende mbele kusaidiana Maisha yao ulimwenguni;
Hata mwisho, ni kuja kwake Yesu,
Wafurahi milele mbinguni.