Nyimbo za Kristo 38
Nasifu Shani ya Mungu
1Nasifu shani ya Mungu, mweneza bahari,
Muumba pia wa mbingu, jua, nyota, mwezi,
Ni tukufu yako shani, mtengeza mambo Ya nyakati na zamani, yasiyo na mwisho.
2Kadri ya nionayo, ya kusifu Mungu;
Nchi niikanyagayo, na hayo mawingu;
Hakuna hata unyasi, usiokuza;
Na upepo wavumisha, au kutuliza.
3Nami kwa mkono wako, naongozwa sawa,
Ni pato nikusifupokukwomba ni dawa;
Umenizingira nyuma, na mbele baraka;
Maarifa ya ajabu!
Yanishinda mimi!