Skip to content

Nyimbo za Kristo 37

Pendo Lako, Ee Mwokozi

Studio

1Pendo lako,
Ee Mwokozi,
Hushinda pendo zote!
Kaa nasi, ndani yetu,
Furaha ya mbinguni.
Yesu, u rehema tupu,
Safi, na kusamehe,
Mfariji mwenye huzuni Ziondoe machozi.

2Roho yako ya upendo Tuma kwa kundi lako;
Hebu tuirithi raha,
Iliyoahidiwa.
Uondoe moyo mbaya,
U Mwanzo, tena Mwisho;
Timiza imani yetu,
Ilituwekwe 'huru.

3Yesu, uje kwetu sasa,
Tupokee huruma;
Rudi kwetu, tena kamwe Usituache pekee.
Tungekutukuza leo, pamoja na malaika,
Imba na kutoa sifa,
Ingia kwa ibada.

4Sasa,
Bwana, kazi yako,
Imalize moyoni;
Takasa hekalu lako,
Wokovu kamilisha!
Safisha viumbe vyako Katika wakati huu;
Tupumzike 'toka dhambi,
Tuingie mbinguni.

Pendo Lako, Ee Mwokozi – Nyimbo za Kristo 37 lyrics | Advent Hymnals