Nyimbo za Kristo 47
Ni Heri Kifungo
1Ni heri kifungo Kinachotufunga Mioyo yetu kwa upendo Pendo la Kikristo.
2Mbele ya Baba Tunatoa sala;
Hofu, nia, masumbufu Yetu ni moja.
3Tunavishiriki Matata na shida,
Na mara nyingi twatoa Chozi la fanaka.
4Tunapoachana Moyoni twalia;
Lakini tutakutana Mwisho mbinguni.