Skip to content

Nyimbo za Kristo 49

Ninaye Rafiki

Studio

1Ninaye rafiki naye Alinipenda mbele;
Kwa kamba za pendo lake Nimefungwa milele.
Aukaza moyo wangu,
Uache ugeuzi,
Ninakaa ndani yake,
Yeye Kwangu, milele.

2Ninaye Rafiki ndiye,
Aliyenifilia;
Alimwaga damu yake,
Kwa watu wote pia.
Sina kitu mimi tena,
Nikiwa navyo tele,
Pia vyote ni amana,
Ndimi wake milele.

3Ninaye Rafiki naye,
Uwezo amepewa;
Atanilinda mwenyewe,
Juu 'tachukuliwa;
Nikitazama mbinguni,
Hupata nguvu tele;
Sasa natumika chini,
Kisha juu milele.

4Ninaye Rafiki naye,
Yuna na moyo mwema;
Ni Mwalimu,
Kiongozi,
Mlinzi wa daima;
Ni nani wa kunitenga,
Na mpenzi wa mbele?
Kwake nimetia nanga, ndimi wake milele.