Skip to content

Nyimbo za Kristo 52

Nipe Biblia

Studio

1Nipe Biblia nyota ya furaha, wapate nuru wasafirio;
Hakuna la kuzuia amani,
Kwani Yesu alituokoa.

RefrainNipe Biblia neno takatifu,
Nuru yako itaniongoza,
Sheria na ahadi na upendo,
Hata mwisho vitaendelea.

2Nipe Biblia nihuzunikapo ikinijaza moyoni dhambi;
Nipe neno zuri la Bwana Yesu,
Nimwone Yesu Mwokozi wangu.

3Nipe Biblia nipate kuona, hatari zilizo duniani;
Nuru ya neno lake Bwana Yesu,
Itaangaza njia ya kweli.

4Nipe Biblia taa ya maisha;
Mfariji tunapofiliwa;
Unionyeshe taa ya mbinguni,
Nione utukufu wa Bwana.

Nipe Biblia – Nyimbo za Kristo 52 lyrics | Advent Hymnals