Nyimbo za Kristo 51
Kuwa Na Yesu Mwokozi
1Yesu Mwokozi, kwa hakika,
Hunipa furaha na amani;
Mrithi wa wokovu wake,
Natakaswa kwa damu yake.
RefrainHabari hiyo wimbo wangu,
Daima nitamsifu Yesu.
Habari hiyo wimbo wangu,
Daima nitamsifu Yesu.
2Nijitoapo nina raha,
Na kwa imani namwona Bwana;
Aniletea malaika,
Wananilinda, niokoke.
3Hali na mali anitwaa,
Katika Yesu nabarikiwa;
Nikimgoja kwa subira,
Wema wake unanitosha.