Nyimbo za Kristo 56
Waponye Watu
1Walio kifoni, nenda waponye.
Uwatoe walio shimoni;
Wanaoanguka uwainue;
Habari njema uwajulishe.
RefrainWalio kifoni waokoeni,
Mwokozi yuko huwangojea.
2Wajapokawia anangojea Awasubiri waje tobani;
Mwokozi hawezi kuwadharau,
Huwasamehe tangu zamani.
3Na ndani ya moyo wa wanadamu Huwapo shida, tena huzuni;
Lakini kwa Yesu kuna rehema Kuwaponya na kuwaokoa.
4Walio kifoni, nenda waponye Kazi ni yetu, zawadi iko;
Nguvu kuhubiri Bwana hutoa Kwa subira tuwavute sasa.