Nyimbo za Kristo 61
Bwana Nami
1Nimemwona rafiki wa thamani kubwa,
Ananipenda kwa 'pole, kwa pendo amini:
Kuishi kutengwa naye, la, huki siwezi,
Tunakaa pamoja:
Bwana nami.
2Pengine nimechoka, mimi mdhaifu,
Ndipo ninamtegemea, alivyoalika;
Huniongoza njiani, pahali pa nuru,
Twatembea pamoja:
Bwana nami.
3Namweleza huzuni, na furaha yangu,
Vile ninavyosumbua, vinavyopendeza;
Huniagiza kutenda, yanayonipasa,
Twazungumza pamoja:
Bwana nami.
4Ajua natamani, kuwavuta watu,
Hivyo ananipeleka, kutangaza Neno;
Nitangaze pendo lake, kwa nini akafa;
Twahubiri pamoja:
Bwana nami.