Skip to content

Nyimbo za Kristo 59

Fanyeni Kazi Zenu

Tune: Church Hymnal 446

1Fanyeni kazi zenu, usiku si mbali;
Kesheni saa zenu vumilieni;
Kwa Yesu tumikeni na hiyo injili.
Sana wahubirini watu wa mbali.

2Fanyeni kazi zenu, giza yasongea;
Na wengi wenzi wenu wamo gizani.
Msipoteze moja dakika ni hizi:
Bwana atarejea mwisho wa kazi.

3Fanyeni kazi zenu, hivi jua lachwa;
Wote walio kwenu‿apenda Mungu:
Na sisi tumjuaye na tuwafundishe‿Ili Yesu ajaye tumfurahishe.