Skip to content

Nyimbo za Kristo 7

Mungu Msaada Wetu

O God, Our Help in Ages Past

Tune: Church Hymnal 81

1Mungu Msaada wetu,
Tangu miaka yote;
Ndiwe tumaini letu la zamani zote.

2Kivuli cha kiti chako ndiyo ngome yetu,
Watosha mkono wako ni ulinzi wetu.

3Kwanza havijakuwako nchi na milima,
Ndiwe Mungu; chini yako twakaa salama.

4Na miaka‿elfu ni kama siku moja kwako;
Utatulinda daima, tu wenyeji wako.

5Bwana msaada wetu tangu miaka yote,
Mlinzi wetu na ngome, daima, milele.