Skip to content

Nyimbo za Kristo 85

Salama Tumepita

Studio

1Salama tumepita, safarini juma hii,
Tumwendee Mwokozi, atubariki sasa:
Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma;
Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma;

2Utupe nuru leo toka hazina yako;
Ondoa dhambi zetu, tupokee na pendo;
Mikono yapumzika, tuishi ndani yako,
Mikono yapumzika, tuishi ndani yako,

3Twakusanyika hapa, tusifu jina lako;
Ukaribie kwetu, tupe neema Bwana;
Utamu tusikize, wa raha ya milele:
Utamu tusikize, wa raha ya milele:

4Injili yako leo, ishike wenye dhambi;
Itupe nguvu nyingi, iponye wenye shida;
Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe.
Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe.