Nyimbo za Kristo 10
Kristo Wa Neema Zote
1Kristo wa neema zote imbisha moyo wangu Mifulizo ya Baraka inaamsha shangwe kuu.
Unifunze nikupende, nikuandame kote,
Moyo wangu ukajae furaha na tumaini.
2Namshukuru sana Bwana, aniwezesha huku.
Salama aniongoza hata kule nyumbani.
Yesu alinitafuta njiani mbali kwake,
Akatoa damu yake nipone hatarini.
3Kweli mimi mwiwa mkubwa wa neema daima;
Wema wako unifunge zaidi kwako Bwana.
Ili nisivutwe tena kukuacha, ee Mponya,
Nitwalie moyo wangu uwe wako kamili.