Skip to content

Nyimbo za Kristo 23

Yesu Furaha Ya Moyo

Studio

1Yesu, furaha ya moyo!
Hazin'ya pendo, na nuru.
Yote yatupendezayo, yasilinganishwe nawe.

2Kweli yako ya daima, wawajibu wakuitao,
Ni siku zote u mwema kwao wakutafutao.

3U Mkate wa uzima, kupokea ni baraka,
Twanywa kwako u kisima roho zikiburudika.

4Mwokozi twakutamani, kwako roho hutulia;
Twakushika kwa imani, nawe watubariki.

5Yesu, ndiwe kwetu mwanga, tufurahishe daima;
Giza ya dhambi fukuza uwe mwanga wa uzima.