Skip to content

Nyimbo za Kristo 112

Wewe Umechoka Sana

Studio

1Wewe umechoka sana?
Wataka raha?
Kwake Yesu utapata Msaada.

2Alama anazo Yeye?
Sana!
Makovu Ya mikono, na miguu,
Na mbavu.

3Naye amevikwa taji Kichwani Mwake?
Taji, kweli, alivikwa Miiba!

4Huku nikimfuata,
Nipate nini?
Maonjo nje, na ndani Amani.

5Kwamba namwandama yeye,
Mwisho ni nini?
Kurithi furaha naye Milele.