Skip to content

Nyimbo za Kristo 114

Yesu Nataka Kutakaswa Sana

Studio

1Yesu Mwokozi ili nitakaswe, nataka moyo uwe enzi yako.
Ukiangushe kilichoinuka unioshe sasa niwe mweupe.

RefrainMweupe tu, ndiyo mweupe,
Ukiniosha nitakuwa safi.

2Bwana Yesu sasa unitazame, unifanye niwe dhabihu hai.
Najitoa kwako, na moyo, vyote; unioshe sana niwe mweupe.

3Bwana kwa hiyo nakuomba sana, nakwongojea miguuni pako,
Wanaokuja hutupi kamwe, unioshe sasa niwe mweupe.