Skip to content

Nyimbo za Kristo 118

Nilipotoka Kabisa

Studio

1Nilipotoka kabisa, sasa narudi;
Nikakawia dhambini,
Bwana narudi.

RefrainNarudi nyumbani: daima kwako.
Kwa upendo nipokee:
Naja nyumbani.

2Nikasusurika sana, sasa narudi;
Mwenye uchungu natubu,
Bwana narudi.

3Nimechoka maovuni, sasa narudi;
Pendo lako lanivuta,
Bwana narudi.

4Ndilo tumaini langu, sasa narudi;
Yesu alinifilia,
Bwana narudi.

5Damu yake yanitosha, sasa narudi;
Unioshe kenyekenye,
Bwana narudi.