Skip to content

Nyimbo za Kristo 128

Taamini Nitii Pia

Trust and Obey

Tune: Church Hymnal 582

1Namwandama Bwana kwa‿alilonena,
Njia zangu huning'azia;
Na nikimridhisha atanidumisha,
Taamini nitii pia.

RefrainKuamini,
Njiani pweke ni hii
Ya furaha kwa
Yesu‿Amini‿ukatii.

2Giza sina kwangu wala hata wingu,Yeye mara huviondoa;
Oga, wasiwasi, sononeko, basi;
Huamini nitii pia.

3Masumbuko yote, sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipia;
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki.
Taamini nitii pia.

4Mimi sitajua raha sawasawa‿Ila yote Yesu kumtoa:
Napata fadhili na radhi kamili,
Taamini nitii, pia.

5Nitamfurahia na kumtumaini,
Majumbani na njia-njia‿Agizo natenda; nikitumwa hwenda,
Huamini, nitii pia