Skip to content

Nyimbo za Kristo 130

Yesu Kwetu Ni Rafiki

Studio

1Yesu kwetu ni rafiki, hwambiwa haja pia:
Tukiomba kwa Babaye, maombi asikia:
Lakini twajikosesha, twajitweka vibaya:
Kama tulimwomba Mungu, dua alisikia.

2Una dhiki na maonjo?
Unamashaka pia?
Haifai kufa moyo, dua atasikia.
Hakuna mwingine Mwema, wa kutuhurumia:
Atujua tu dhaifu: maombi asikia.

3Je, hunayo hata nguvu, huwezi kwendelea,
Ujapodharauliwa, ujaporushwa pia.
Watu wakikudharau, wapendao dunia,
Hukwambata mikononi, dua atasikia.