Nyimbo za Kristo 135
Kwa Maombi Nachangamka
1Saa heri ya maombi, sasa kwako tunarudi,
Sumbuku ya kuondoa, shida zetu na pungufu.
Taabuni mara nyingi, roho zetu zimepona,
Mashaka tumeshinda, wakati wa saa tamu.
2Saa heri ya maombi, twapeleka dhiki zetu Kwake aliyeahidi kubariki wenye haja.
Huagiza tumwendee, tutegemee neno lake,
Hivyo tumwekee yote, wakati wa saa tamu.
3Saa heri ya maombi, tutazidi kuingia,
Bomani mwetu na ngome, hata tuishapo mwendo.
Yesu atatusikia, tutamtafuta daima,
Na tutakapokutana tutamwona, saa tamu!