Skip to content

Nyimbo za Kristo 137

Saa Heri Ya Sala

Studio

1Saa heri ya sala tunapojidhili,
Kama tukija kwake Yesu rafiki;
Tukiwa na imani kwamba yu mlinzi,
Waliochoka sana watapata raha.

RefrainSaa ya sala, iliyo heri;
Waliochoka sana watapata raha.

2Saa heri ya sala, ajapo Mwokozi,
Ili awasikie watoto wake.
Hutwambia tuweke miguuni pake Mizigo yetu yote: tutapata raha.

3Saa heri ya sala, wawezapo kuja Kwa Bwana Yesu wanaojaribiwa;
Moyo wake mpole, atawarehemu;
Waliochoka sana watapata raha.

4Saa heri ya sala tutakapopewa,
Mibaraka ya roho, tukimwamini;
Kwa kuamini kweli hatutaogopa;
Waliochoka sana watapata raha.

Saa Heri Ya Sala – Nyimbo za Kristo 137 lyrics | Advent Hymnals