Skip to content

Nyimbo za Kristo 146

Twae Wangu Uzima

Studio

1Twae wangu uzima,
Sadaka ya daima;
Twae saa na usiku,
Zikutukuze huku.
Zikutukuze huku.

2Twae mikono nayo,
Ifanye upendavyo,
Twae yangu miguu,
Kwa wongozi wako tu.
Kwa wongozi wako tu.

3Twae sauti yangu,
Niimbe kwa Mungu tu;
Itwae na midomo,
Ijae neno lako.
Ijae neno lako.

4Twae dhahabu pia,
Na yote ya dunia;
Twae yangu hekima,
Upendavyo tumia.
Upendavyo tumia.

5Nia itwae,
Mungu,
Haitakuwa yangu;
Twae moyo; ni wako,
Uwez'makazi yako.
Uwez'makazi yako.

6Twae mapenzi yangu,
Sifa za moyo wangu;
Twae kabisa nafsi,
Niwe wako halisi.
Niwe wako halisi.