Nyimbo za Kristo 147
Uishi Ndani Yangu
1Tawala ndani yangu,
Ee Yesu,
Mfalme.
Uwe kwangu majibu Kwa maswala yangu;
Uishi ndani yangu,
Wewe, mwongozi Utumishi ni wangu,
Wako utukufu.
2Hekalu nimetoa,
Umelisafisha;
Sasa fahari yako Imulike ndani;
Dunia iwe kimya,
Mwili sasa uwe Mtumwa mtulivu Wa kukutii tu.
3Viungo vyake mwili,
Vyote vikungoja Tayari vikiitwa Kwenda, kusimama;
Bila manunguniko Au malaumu,
Au kusumbuliwa,
Pasipo majuto.
4Niwe na utulivu Pasipo haraka;
Tayari kungojea Maagizo yake.
Tawala ndani yangu.
Ee Yesu,
Mfalme,
Uwe kwangu majibu Kwa maswali yote.