Skip to content

Nyimbo za Kristo 158

U Mwendo Gani Nyumbani?

Studio

1U mwendo gani nyumbani?
Mlinzi akanijibu,
Usiku sasa waisha, macheo karibu.
Usihuzunike tena, bali ulemee mwendo Hata ushike ufalme kule mwangani juu.

2Na tena niliuliza, nchi yote ikajibu;
Sasa mwendo watimika, milele karibu.
Usihuzunike tena, ishara kuu zasonga Na viumbe vyangojea sauti ya Bwana.

3Nikamwuliza shujaa, ndivyo kanitia moyo:
Shikilia mapigano, kitambo yaisha.
Usihuzunike tena, kazi ifanywe kwa moyo;
Tumeahidiwa tunu tuishapo shinda.

4Siyo mbali na nyumbani!
Fikira tamu njiani,
Latupoza roho, nalo lafuta machozi.
Usihuzunike tena, kitambo tutakutana Wenye furaha kamili nyumbani mwa Baba.

U Mwendo Gani Nyumbani? – Nyimbo za Kristo 158 lyrics | Advent Hymnals