Nyimbo za Kristo 151
Huniongoza Mwokozi
1Huniongoza Mwokozi, ndipo nami hufurahi,
Niendapo pote napo, ataniongoza papo.
RefrainKuongoza hunishika; kwa mkono wa hakika;
Nitaandamana naye Kristo aniongozaye.
2Pengine ni mashakani nami pengine rahani;
Ni radhi, ijapo yote, yupo nami siku zote.
3Mkono akinishika kamwe sitanungunika;
Atakachoniletea ni tayari kupokea.
4Nikiisha kazi chini sitakimbia mauti;
Kuishinda ni ya hakika nikiongozwa na Baba.