Nyimbo za Kristo 152
Karibu Na Wewe, Mungu Wangu
1Karibu na wewe,
Mungu wangu;
Karibu zaidi,
Bwana wangu.
Siku zote niwe karibu na wewe,
Karibu zaidi,
Mungu wangu.
2Mimi nasafiri duniani,
Pa kupumzika sipaoni,
Nilalapo niwe karibu na wewe,
Karibu zaidi,
Mungu wangu.
3Yote unipayo yanivuta;
Pa kukaribia nitapata;
Na nielekezwe karibu na wewe;
Karibu zaidi,
Mungu wangu.
4Na kwa nguvu zangu nikusifu,
Mwamba, uwe maji ya wokovu;
Mashakani niwe, karibu na wewe,
Karibu zaidi,
Mungu wangu.
5Na nyumbani mwa juu,
Baba yangu;
Nikinyakuliwa toka huko,
Kwa furaha niwe pamoja na wewe,
Karibu zaidi Mungu wangu.