Skip to content

Nyimbo za Kristo 155

Njiani Huniongoza

Studio

1Njiani huniongoza Yesu wangu,
Mwokozi:
Rehema hatapunguza,
Milele Kiongozi.
Ina raha kwandamana Duniani daima:
Nijaposumbuka sana, yeye hutenda vyema;
Nijaposumbuka sana, yeye hutenda vyema.

2Njiani huniongoza,
Hupunguza matata;
Nikiungua hupoza,
Na njaani nashiba.
Lichokapo guu langu,
Nguvu zikapungua,
Jiwe lilo mbele yangu hunibubujika ;
Jiwe lilo mbele yangu hunibubujika .

3Njiani huniongoza Kwa pendo zilizo kuu,
Mwisho atanituliza Kwake Baba yangu juu,
Nikivikwa kutokufa,
Nikae na Mwokozi,
Nitamsifu sana; sifa:
Kweli ni Kiongozi;
Nitamsifu sana; sifa:
Kweli ni Kiongozi.