Nyimbo za Kristo 156
Uniongoze Jehova
1Uniongoze,
Yehova,
Ni msafiri chini;
Ni mnyonge, u hodari,
Nilinde kwa mkono.
Unitunze, unilinde,
Unionyeshe njia!
Unionyeshe njia!
2Na kisima cha uzima,
Maji ya utabibu,
Fungua kwa moyo wangu,
Ninywe na kuponyeka!
Uninyweshe, unilishe,
Hata nimetosheka,
Hata nimetosheka.
3Wakati wa kuuvuta,
Ule mto Yordani,
Hofu yangu ufariji,
Nione uso wako.
Nyimbo shangwe, nyimbo shangwe,
Nitaimba daima,
Nitaimba daima.