Nyimbo za Kristo 157
Mfalme Yu Mlangoni
Tune: Church Hymnal 546
1Mfalme yu mlangoni,
Ndiye‿aliyetufia;
Mara wote wampendao atawakusanya.
RefrainYuaja, yuaja, mlangoni anasimama;
Anakuja, anakuja,
Kuja kwake karibu.
2Dalili za kuja kwake
Zinazidi kutimizwa;
Karibuni wateule watamlaki Bwana.
3'Sitafute duniani amani wala furaha,
Mpaka Bwana arudi dhambi kuondoa.
4Tutakaa na Mwokozi
Makaoni ya milele;
Daima tutafurahi kuwa watu wake.