Skip to content

Nyimbo za Kristo 172

Mfalme Ajapo

Tune: Church Hymnal 537

1Mfalme wetu atuita tukae karamuni kwake;
Itakuwaje nasi kule Bwana ajapo?

RefrainBwana ajapo, ndugu, Bwana ajapo!
Itakuwaje na sisi, Bwana akija?

2Atavikwa vizuri sana, taji badala ya miiba;
Kweli tokeo la fahari Bwana ajapo.

3Kwa furaha‿awakubali wenye mavazi ya arusi;
Tu wa heri tukimridhisha Bwana ajapo.

4Kutakuwako na utengo: watalia waliomwasi;
Cha kutisha kitambo kile Kristo ajapo!

5Mfalme utupe neema sisi tunapokungoja,
Tusiogope kukuona ujapo Bwana.