Nyimbo za Kristo 173
Hatujui Saa
1Hatujui saa ya kuja kwa Bwana,
Lakini dalili zasema karibu,
Atakaporudi, lakini kwa kweli,
Hatujui saa.
RefrainAtakuja, kwa vile tukeshe;
Atakuja Mwokozi,
Aleluya!
Atakuja kwa fahari ya Baba yake,
Hatujui saa.
2Pana nuru kwao wapendao haki,
Pana kweli katika Chuo Cha Mungu;
Unabii hufundisha kuja kwake,
Hatujui saa.
3Tutakesha tutaomba daima Tutafanya kazi mpaka akija;
Tutaimba na tutasoma ishara,
Hatujui saa.