Nyimbo za Kristo 174
Tukimngojea
Tune: Church Hymnal 542
1Sijui‿atakapokuja,
Mchana au usiku;
Labda sa-a ya alasiri.
Pengine ni alfajiri.
Hutwambia tuwe tayari,
Ta-a zetu tusizime;
Ili ajapo atukute;
Tuwe tukimngoja Yeye.
RefrainTukimngojea,
Tukimngojaa,
Tukimngojaa,
Twakesha, twamngoja Yeye.
2Nakumbuka huruma zake,
Bei ya wokovu wetu;
Aliacha nyumba tukufu‿Awafilie wabaya.
Ninadhani‿itampendeza,
Kama sisi watu wake,
Tukionyesha pendo letu,
Tuwe tukimngoja Yeye.
3Ee Yesu, Mwokozi mpendwa,
Wajua nalihifadhi Tumaini la kukuona.
La kukaribishwa nawe.
Ukija kwa watu wengine,
Kama mhukumu wao,
Kwangu‿utakuwa rafiki,
Nakesha, nakungojea.