Skip to content

Nyimbo za Kristo 190

Raha Yangu Yote, Bwana

Tune: Advent Hymnals (Dundee)

1Raha yangu yote, Bwana, i mbavuni pako;
Mimi sina haja tena ila kifo chako.

2Mwokozi uliyekufa, nawe ndiwe Mungu,
Kifo chako ni kwa dhambi, ziondoe zangu.

3Nioshe na niwe wako, nawe uwe wangu;
Nioshe damuni mwako liwe fungu langu.

4Nioshe si miguu tu, osha tangu nyayo,
Hata kichwa changu juu, na ndani ya moyo,

5Na iwe kafara damu nifanyapo kazi,
Hata imani itimu, nikwone, Mwokozi.