Skip to content

Nyimbo za Kristo 192

Mwamba Wenye Imara

Studio

1Mwamba wenye imara, kwako nitajificha!
Maji hayo na damu yaliyotoka humu,
Hunisafi na dhambi,
Hunifanya mshindi.

2Kwa kazi zote pia sitimizi sheria,
Nijapofanya bidii, nikilia na kudhii,
Hayaishi makosa; ndiwe wa kuokoa.

3Sina cha mkononi, naja msalambani,
Nili tupu, nivike; ni mnyonge, nishike;
Nili mchafu, naja, nioshe nisijafa.

4Nikungojapo chini, na kwenda kaburini,
Nipaapo mbinguni na kukwona enzini,
Roho yangu na iwe rahani mwako wewe.